Kitulo FM

Wananchi elfu 15 Waanza kunufaika na mradi wa Maji Matamba-Kinyika

January 11, 2023, 7:43 pm

Makabidhiano ya Mradi yakifanyika katika ukumbi wa FEMA, Matamba

Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA) imetekeleza mradi wa Zaidi ya Bilioni moja katika Tarafa ya Matamba na kuukabidhi kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Makete Ruwasa mradi huo unatambulika kwa jina la Matamba-Kinyika

Makabidhiano ya Mradi huo yamefanyika jana katika Kijiji cha Matamba ukumbi wa FEMA mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda.

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda ameishukuru IRUWASA kwa kutekeleza mradi huo mkubwa na sasa kuamua ukabidhiwe kwa Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Wilaya ya Makete RUWASA kwa umaliziaji wa mradi huo ambao umefikia 97%

Mkurugenzi wa Wizara ya Maji Bi. Joyce Msiru amewataka RUWASA kuendelea kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi na kuweka mikakati ya kuhakikisha maji hayapotei kwa kufanya ukarabati wa miundombinu chakavu

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya watumia Maji Matamba Bi. Faraja amesema mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa Tafara ya Matamba ambao wameondokana na uhaba wa maji kwa sasa huku akiongeza kuwa endapo watafanikiwa kufunga dira za maji itasaidia kuwepo na matumizi mazuri ya maji kwa wateja

Mhandisi David Pallanyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisaf na usafi wa Mazingira Iringa amesema Mradi huo umeanza kunufaisha wakazi takribani 15,320 ukiwa na wastani wa ujazo wa Lita 1,218,000 kwa siku