Kitulo FM

Elimu ya Utunzaji wa Mazingira kuanza kutolewa Liganga na Mchuchuma Ludewa

January 11, 2023, 7:47 pm

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ludewa Sunday Deogratias

Kufuatia kuanza kwa miradi midogo ya uchimbaji madini ya makaa ya mawe wilayani Ludewa mkoani Njombe huku miradi mikubwa ya Liganga na Mchuchuma ikitarajiwa kuanza hivi karibuni shirika lisilo la kiserikali Umbrella of Women and Disabled organization (UWODO) imewasili wilayani humo kwa lengo la kuendesha mradi wa utoaji elimu juu ya utunzaji mazingira na uoto wa asili katika maeneo hayo ya miradi.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo wa utunzaji mazingira na uoto wa asili Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Sunday Deogratias amelipongeza shirika hilo kwa kuwa limekuja katika kipindi ambacho kunauhitaji hasa wa elimu hiyo.

Hamis Kassapa ni Mkurugenzi wa shirika hilo la UWODO ameeleza namna ambavyo mazingira yamekuwa yakiharibiwa katika machimbo mbalimbali hivyo amesema elimu hiyo itatolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha kata ya Luilo na Nkomang’ombe huku awamu ya pili ikihusisha kata ya Mundindi.

Mradi huo ambao umeonekana kupokelewa vyema na viongozi mbalimbali wa wilaya na kata husika akiwemo diwani wa kata ya Nkomang’ombe John Maganga pamoja na diwani wa kata ya Luilo Mathei Kongo.