Mkuu wa Mkoa awahimiza wazazi kupeleka watoto shule
Kitulo FM

Watoto wote waende Shule-Rc Mtaka

January 6, 2023, 11:40 am

 

Mkuu wa Mkoa awahimiza wazazi kupeleka watoto shule

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka amewataka wazazi/walezi wenye watoto waliofikia umri wa kuanza darasa la kwanza kuwapeleka shule ifikapo tarehe 9, Januari 2023.

Akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Njombe kwenye Baraza la 7 la wafanyabiashara lililofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe tarehe 5 Januari 2023 amesema lazima mzazi kutambua umuhimu na haki ya mtoto kupata Elimu katika Mazingira rafiki na kupewa vifaa vyote muhimu kwa mahitaji ya elimu.

Mtaka ameongeza kuwa Serikali imejenga madarasa katika shule mbalimbali zilizokuwa na upungufu hivyo hakuna haja ya mzazi au Mlezi kumkosesha haki ya Elimu mtoto.

Amewataka wazazi na walezi kuwanunulia vifaa vya shule watoto wao na hata ambao watashindwa wahakikishe watoto wanapelekwa shule kuanza masomo.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa amewaomba wafanyabiashara kuacha tabia ya kupandisha bei za bidhaa za wanafunzi badala yake wauze vifaa hivyo kwa bei halisia ikiwemo nguo, madaftari n.k