Waziri Kijaji
Kitulo FM

Wakurugenzi simamieni Malipo ya Ushuru wa Mbao wa 3%- Waziri Kijaji

January 6, 2023, 12:00 pm

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dk Ashatu Kijaji akizungumza Mkoani Njombe kwenye Baraza la wafanyabiashara

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dk Ashatu Kijaji amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe kuhakikisha inakusanya mapato ya Mbao kwa 3% kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Serikali na siyo shilingi 100 kwa kila ubao kama ilivyo sasa kwa baadhi ya Halmashauri

Hii ni baada ya wafanyabiashara mbalimbali kuomba Mapato ya ushuru wa Mbao walipie kwa 3% wakati wa Mkutano wa Baraza la wafanyabiashara Mkoa wa Njombe wakiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika Mkutano wa 7 uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe

Waziri Kijaji amewasihi wakurugenzi kutoka Halmashauri ya Wilaya Makete, Wanging’ombe, Ludewa, Njombe, Halmashauri ya Mji Makambako kuhakikisha wafanyabishara wanalipa ushuru kwa 3% kila wanapofanya biashara ya usafirishaji wa Mbao katika maeneo hayo.

Wafanyabiashara hao wamesema wamekuwa wakitozwa ushuru wa shilingi 100 kwa kila ubao ilihali Serikali imeweka utaratibu wa kutoza 3% kwa kila ubao na kuwaomba wakurugenzi kusimamia jambo hilo la asilimia ili kuhakikisha wafanyabiashara wote wanalipa fedha hizo kwa uaminifu.