Kitulo FM

Wahamiaji haramu wakamatwa Makete

November 10, 2021, 3:40 pm

Wahamiaji haramu 18 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa eneo la kusajanilo kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe

John Hindi ni kamishna msaidizi mwandamizi wa uhamiaji Mkoa wa Njombe amesema wahamiaji hao walikuwa wanaelekea nchi jirani ya Malawi

Aidha amewataka wananchi Wilaya ya Makete kuendelee kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama pindi wanapowaona wahamiaji haramu katika Maeneo yao ili kuthibiti vitendo hivyo

Picha ya wahamiaji haramu

Kwa upande wake Kamanda wa polisi Mkoa Njombe Hamiss Issa amewaonya wanaofanya kazi ya usafirishaji wa wahamiaj haramu kuacha mara Moja tabia hiyo kwani Sheria itachukua mkondo wake Dhidi yao.