Kitulo FM

Ahukumiwa Miaka 30 Jela

November 9, 2021, 2:17 pm

Frank sanga (23) mkazi wa iniho Wilayani Makete Mkoani Njombe amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka (13) (jina limehifadhiwa) wa kijiji cha Iniho

Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 7 oktoba,2021 katika kijiji cha iniho mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka  mtoto huyo wa shule ya msingi iniho ambalo  kosa hilo ni  kinyume na kifungu cha 130 (1)(2e)cha  sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2019

Picha hii ni Mfano wa Mtu aliyefungwa

Aidha mshtakiwa aliiomba Mahakama iweze kumpunguzia adhabu kwa kuwa anaishi na bibi yake ambaye anamtegemea

Hata hivyo upande wa mashtaka imeiambia mahakama kuwa ili kukomesha vitendo hivyo mshtakiwa anatakiwa kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.