Kitulo FM

WANAFUNZI WAPATA VYETI

October 27, 2021, 10:33 am

Wanafunzi 70 Kidato cha nne Iwawa Sekondari watunukiwa vyeti vya utambuzi wa ushiriki wao kwenye Club ya Wasaidizi wa Kisheria shuleni (Paralegal School Club)

Wanafunzi hao kwa miaka miwili wamekuwa wakipata mafunzo kutoka kwa Wasaidizi wa Kisheria Kata ya Iwawa na Ofisi ya Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete (MAPAO), ambapo nao wamekuwa wakitoa Elimu hiyo kwa Wanafunzi wenzao shuleni hapo

Wanafunzi wa Iwawa Sekondari.

“Tunawapongeza kwa utoaji wa Elimu ya msaada wa Kisheria mliokuwa mkiutoa kwa Wanafunzi wenzenu, lakini muendako mkawe Wasaidizi vilevile kulingana na kile tulichowafunza” Mkurugenzi Mtendaji Shirika la wasaidizi wa Kisheria Makete Mch. Denis Sinene

Wanafunzi hao kwa Umoja wao wamesema Elimu hii imekuwa msaada mkubwa kwao na Wanafunzi wengine, hivyo Club hiyo ni vema ikaendelea kuwepo ili wenzao wanaobaki waendelee kunufaika.