Kitulo FM

SHULE YA UONGOZI

October 26, 2021, 6:47 pm

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (MNEC) Ndg.Japhari Kubecha
atoa shule ya Uongozi kwa Vijana nchini

Akizungumza na Kitulo FM, Kubecha amesema kijana ni mtu muhimu kwenye taifa hili husani katika uongozi kwani asilimia kubwa ya watanzania ni vijana na kijana ni kizazi kitakacho kuja kurithi nchi

Japhari Kubecha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (MNEC)

“Baadhi ya wazee hawakubali kustaafu kwa sababu walikuwa na tamaa, ulafi na uroho wa madaraka kwani kustaafu ni kuamua kurithisha mambo uloyokua unayafanya kwa maana hiyo unabaki kuwa rejea hivyo vijana waendelee kuaminiwa katika nafasi za uongozi sio mpaka wawe wazee”

Kubecha amesema kwa sasa asilimia 57 ya madiwani nchi nzima ni vijana na katika Bunge asilimia zaidi 60 ni vijana hivyo vijana wamepiga hatua katika Uongozi na tunatariji mihimili ya nchi vijana wanapata nafasi zaidi

Pia amewataka vijana kuchangakia fursa ya mikopo inayotolewa kwenye Halmashauri na kuwataka kuwa na mikakati ya pamoja ili kupata maendeleo yao binafsi na nchi kwa ujumla