Kitulo FM

WALIMU OENI

October 22, 2021, 1:27 pm

Walimu wa Kiume shule za Sekondari Wilayani Makete Mkoani Njombe wameshauriwa kuoa ili kupunguza tamaa zinazoweza kuwashawishi kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe (katikati),kulia ni Mwalimu Prisca Myala Afisa elimu wilaya ya Makete wakizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Lupila

Hii ni katika kupambana na mimba kwa wanafunzi wa kike shule za Sekondari katika Wilaya ya Makete

Akizungumza na walimu shule ya sekondari Lupila Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete Ndg. Willium Makufwe amewasihi walimu kutojihusisha na vitendo viovu kimapenzi na wanafunzi wao.

Kuhusu shule kutoa matokeo mazuri baada ya wanafunzi kuhitimu, Makufwe amewasihi walimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kuwa haki zao zote kutoka serikalini wamezipata hivyo wawe walimu wa Matokeo chanya

Sauti ya Mkurugenzi akizungumzia kuhusu Walimu kuwajibika

Mkuu wa shule ya sekondari Lupila Mwalimu Abkasa Ngwale amesema katika shule yake haijawahi kutokea Mwalimu kujihusisha kimapenzi na Mwanafunzi kwa kuwa walimu hao wamekuwa walezi wa wanafunzi wakati wote.