Karagwe FM

Wananchi Misenyi wapewa maelekezo Maalumu ya Sensa.

13 August 2022, 12:12 pm

Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Wilson Sakulo amesema kuwa hakuna malipo yatakayotolewa kwa wananchi wakati wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022.

Kanali Sakulo ametoa kauli hiyo akiwa Ofisini kwake leo jumamosi tarehe 13 August 2022 wakati akiongea na vyombo vya habari juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sensa pamoja na mchakato wa mafunzo yanayoendelea kwa Makarani, wasimamizi wa maudhi na TEHAMA.

DC Misenyi – Kanali Wilson Sakulo

“Jana tarehe 12 August 2022 wasimamizi wa sensa wanaoendelea na mafunzo walipita katika baadhi ya kaya kufanya majaribio ya kutumia vifaa na kuuliza maswali lakini cha kusikitisha baadhi ya wananchi walitaka kujua kama watalipwa ili watoe taarifa zao” Amesema Sakulo

Aidha Kanali Sakulo amesisitiza kwamba hakuna Mwananchi atakayelipwa fedha ili kutoa taarifa zake kwakuwa zoezi la sensa ni suala muhimu kwa maendeleo ya Taifa hivyo wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi kutokana na Maswali watayoulizwa

Ameongeza kuwa sensa ya watu na makazi inalenga kuiwezesha serikali na wadau wengine kupata takwimu sahihi za watu na makazi ili kuweka mipango ya Maendeleo.