Karagwe FM

Wakuu wa Idara wakalia kuti kavu.

11 March 2022, 8:55 am

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro kuwachukulia hatua  za kiutumishi wakuu wa Idara wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za Manunuzi  kwenye ujenzi wa shule ya Sokoine Memorial High School iliyoko Mkoani Morogoro.

Akiongea na uongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Machi 10 mwaka huu wakati akikagua miradi inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo Waziri Bashungwa amesema kumekuwa na dosari kwenye Manunuzi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.

Waziri Bashungwa akitoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya Mvomero

Amesema  Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero lakini kumekuwa na dosari katika suala zima la manunuzi inayosababisha miradi kukwama na kutomalizika kwa wakati.

Amefafanua kuwa kumekuwa na Dosari kwenye kunukuu bei kabla ya kupatiwa idhini na Mkurugenzi wa Halmashauri ambapo bei hutolewa kwanza kisha idhini ufuata baadaye jambo ambalo amesema halikubaliki katika sheria za manunuzi.

Majengo ya shule ya Sokoine Memorial – Morogoro

Bashungwa amesema kuwa dosari nyingine kuleta kwa mzigo kwanza ndipo local parchasing order inasiniwa ambapo ni kinyume na utaratibu piq utumiaji wa fomu za vivuli badala ya fomu halisi.

Ameendelea kufafanua kuwa dosari nyingine kwa upande wa Manunuzi ni kuwa upo ushahidi inaonyesha uteuzi wa wazabuni kupewa kazi wakati hawaKujaza fomu wakati wa kutafuta mzabuni, hivyo kuonyesha kuwa kuna udanganyifu upande wa Manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

Aidha, amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kufuata sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kuendesha Halmashauri ili wasiingie kwenye matatizo ambayo yanatokana na kwenda kinyume na utaratibu.

Baadhi ya Viongozi wa mkoa Morogoro na wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero