Karagwe FM

Halmashauri ya Missenyi yatoa mkopo shilingi Milioni 294.8

29 January 2022, 10:01 pm

Halmashauri ya Wilaya Missenyi imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi milioni 294.8 kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu

Katika tukio lakukabidhi mikopo hiyo kwa vikundi 50 vya wajasiriamali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Projestus Tegamaisho amesema wataendelea kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kuwezesha Wana Missenyi Kiuchumi hivyo akawataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho akikabidhi hundi kwa wanufaika

Tangu mwaka 2010/2011 mpaka sasa Halmashauri ya Missenyi imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 kwa vikundi vya wajasiriamali 534

Baadhi ya akina mama walionufaika na mkopo
Baadhi ya vijana walionufaika na mkopo huo