Karagwe FM

Madiwani Missenyi waridhia kujenga uwanja wa michezo

24 January 2022, 9:46 pm

Baraza la Madiwani Missenyi limeridhia Ujenzi wa Uwanja wa Michezo na suala hili kuweka katika mpango mkakati wa Maendeleo wa miaka mitano. Katika kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kilichoketi Jumatatu Januari 24, 2022 kwa ajili ya kupitisha mpango Mkakati wa Mwaka 2021/2022 mpaka 2025/2026, Madiwani hao kwa kauli moja wameridhia suala la Ujenzi wa Uwanja huo wa Michezo kuingizwa kwenye Mpango mkakati wa Halmashauri*”Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa miguu na michezo mingine ni kipaumbele chetu Madiwani na wadau wengine, nimeagiza wataalam kuanza mchakato ili tujue mahali patakapojengwa uwanja huo na gharama zinazohitajika”* Amesema Projestus Tegamaisho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Missenyi bw. Projestus Tegamaisho

Baadhi ya Madiwani Yusuf Mzumbe, Rafiu Hussein, Regina Rwamuganga na Robert Nshekanabo wamesema kwamba umefika wakati wa Missenyi kuwa na uwanja wa michezo utakaotumika kama chanzo cha Mapato ya Halmashauri pamoja na kupanua wigo wa masuala mbalimbali yahusuyo michezo

Baadhi ya Madiwani wa Missenyi wakiwa katika mkutano maalumu