Karagwe FM

Miradi ya Maendeleo yatengewa Bilioni 3.3

15 November 2021, 11:30 am

DC Karagwe – Julieth N. Binyura

Zaidi ya shilingi bilioni tatu zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Karagwe kama pesa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwaajili ya mapambano dhidi ya Uviko-19.

Akizungumza na Redio Karagwe Fm sauti ya wananchi Nov 15 mwaka huu,Mkuu wa wilaya Karagwe mwalimu Julieth N. Binyura amesema kuwa pesa hiyo itasaidia kuchochea kasi ya maendeleo na kwamba serikali imeweka utaratibu utakaosaidia kuratibu matumizi kusudiwa ya pesa hizo.

DC Karagwe – Julieth N. Binyura

Mwalimu Binyura ametaja miradi itakayotekelezwa kutokana na pesa hiyo.

Miradi itakayo tekelezwa – DC Binyura

Amesema kuwa pesa hiyo itumike kwaajili ya kutekeleza miradi na siyo kushibisha matumbo ya watu na akatoa wito kwa wasimamizi wa pesa hiyo.

wito wa Dc Binyura

Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya saba (7) zinazounda Mkoa wa Kagera.Wilaya ya Karagwe inapakana na Wilaya ya Kyerwa upande wa Kaskazini, nchi ya Rwanda upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba upande wa Mashariki.

Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.