Karagwe FM

Ngeze achaguliwa kuwa mwenyekiti wa ALAT

29 September 2021, 7:02 am

Mweyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Murshid Ngeze amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa mamlaka ya viongozi wa serikali za mitaa ALAT Taifa katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma.

Mweyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Murshid Ngeze

Akiongea na Radio Karagwe kwa njia ya simu Bw. Ngeze amewashukuru wananchi wa Bukoba waliomchagua kuwa diwani wa kata ya Rukoma na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo nafasi iliyomuwezesha kugombea na hatimaye kupata nafasi hiyo mpya.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa nafasi hiyo itampa fursa ya kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo kwa urahisi tofauti na hapo awali.

Mweyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Murshid Ngeze