Karagwe FM

Wasiojikinga na Covid 19 kukiona cha moto

29 June 2021, 7:41 am

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi.Julieth Binyula ameziagiza Taasisi za Kiserikali na zisizokuwa za Kiserikali kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa COVI 19.

DC Karagwe – Julieth Binyula (kulia)

Binyula amesema hayo kupitia mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataka wafanyabiashara pia kuweka maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono katika maeneo yao ya biashara.

DC Karagwe – Julieth Binyula

Binyula amewatahadharisha wote watakaokiuka maagizo hayo kwamba vyombo vya dola havitasita kuchukua hatua.

Agizo la DC Julieth Binyula.