Kayanga Stendi
Karagwe FM

Wapewa saa 48 kuhamisha vibanda.

26 May 2021, 7:07 pm

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Karagwe Godwin Kitonka amewataka wajasiriamali wanaofanya biashara katika stendi ya Kayanga wilaya Karagwe kuhamisha vibanda vilivyojengwa katika eneo hilo kabla ya May 27 mwaka huu.

Godwin Kitonka – (DED) Karagwe.

Bwana Kitonka ametoa kauli hiyo Mei 26 mwaka huu wakati alipozungumza na Redio Karagwe Fm sauti ya wananchi ambapo amesema kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakijenga vibanda katika eneo hilo bila kufuata utaratibu na kuharibu mandhari ya Mji wa Kayanga.Amesema kuwa atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya vibanda vilivyojengwa katika eneo la Standi hiyo.
Sauti ya (DED) Karagwe Godwin Kitonka.