Misenyi
Karagwe FM

Watano watumbuliwa Misenyi

17 May 2021, 10:16 pm

Viongozi 5 wa Chama Cha Ushirika wa wakulima wa miwa Missenyi UWAMMISE na BUBARE AMCOS wameondolewa kwenye uongozi baada yakukiuka kanuni na taratibu za Ushirika.

Misenyi

Akitangaza kuwaondoa kwenye uongozi Jumatatu Mei 5 mwaka huu ,Afisa Ushirika Wilaya ya Missenyi Gabinus Damiano Mtonga amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya viongozi hao kukiuka kanuni na taratibu za Ushirika wakati kupanga bei ya miwa baina AMCOS na kiwanda cha sukari Kagera Sugar kinachonunua miwa

“Viongozi wa vyama hivi leo tarehe 17/05/2021 nimewakuta wakiwa wanajadiliana juu ya bei ya miwa na kiwanda cha Kagera Sugar pasipo serikali kujua,bila taarifa kufika kwa Mkurugenzi na utaratibu uliotumika unakiuka sheria ya Ushirika hivyo natangaza kuwaondoa kwenye uongozi” Amesema Mtonga

Amefafanua kuwa kwa kufanya majadiliano ya bei kwa ajili ya msimu wa mwaka 2021/2022 wamekiuka kanuni ya vyama vya Ushirika ya mwaka 2014 kifungu cha 76 (1) kinachokataza kuingia Mkataba kabla yakupata idhini ya Mkutano Mkuu na kifungu cha 76 (3) kinachosema kuwa afisa yeyote atakayeingia makubaliano atakuwa ametenda kosa

Afisa Ushirika ametaja majina ya viongozi wa Chama Cha Ushirika wa miwa UWAMMISE kuwa ni Mwenyekiti wa bodi Ahamada Ngemera,Makamu Mwenyekiti Patrick Ishengoma, Wajumbe wa bodi Isack Said,Julius Bukagire pamoja na Mwenyekiti wa BUBARE AMCOS Leonard Deogratias

Amesema kuwa wajumbe hawa wote wasijihusishe na shughuli za Ushirika nakuwa atawaandikia barua rasmi zakuwaondoa kwenye Ushirika nakwamba majadiliano waliyofanya leo na uongozi wa kiwanda ni batili yana mazingira ya rushwa nakumnyonya Mkulima wa miwa.

Afisa Ushirika Wilaya Missenyi Gabinus Damiano Mtonga