WAZIRI BASHUNGWA
Karagwe FM

Waziri Bashungwa awafuturisha Waislamu.

11 May 2021, 12:01 pm

Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa ambaye pia ni waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezi amewafuturisha waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wageni waalikwa huku Futari hiyo ikiambatana na harambee ya ujenzi wa kituo cha afya.

Picha ya pamoja ( Shehe Nasibu Abdul,Waziri Bashungwa na DAS Karagwe)

Shehe wa Wilaya ya Karagwe Nasibu Abdul amesema kuwa mbunge wa jimbo la Karagwe amekuwa na ushirikiano tangu mwanzo na amekuwa karibu na waumini wa dini ya kiislamu na kumuahaidi kuendelea kushirikiana naye.

Shehe Nasibu Abdu – Shehe ( W) Karagwe.

Nae mgeni rasmi katika Futari hiyo mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa ambaye pia ni waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo amesema ushirikiano wa viongozi wa dini ndiyo nguzo muhimu ambayo siku zote imekuwa ikichochea maendeleo ya Karagwe pamoja na Taifa.

Waziri Bashungwa amesema kwenye ujenzi wa kituo cha afya ambacho waumini hao ambacho wanatarajia kukijenga atashirikiana nao kwa kila hatua na kwa kuanza amehaidi kiasi cha sh Millioni moja.

Habari kamili na Ospicia Didace.