Karagwe FM

Miradi yalamba Milioni 96 kwa miezi 3.

11 May 2021, 11:34 am

Zaidi ya shilingi Milioni 96 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Kayanga wilaya Karagwe kwa kipindi cha robo ya mwaka 2021.

Sauti ya diwani kata Kayanga – Geremanus Byabusha

Akizungumza na Redio Karagwe Fm sauti ya wananchi May 11 mwaka huu,Diwani wa kata Kayanga bwana Geremanus Byabusha amesema pesa hiyo iliyotumika kutekeleza miradi inayogusa Afya,Elimu na miundombinu imetokana na michango ya wananchi pamoja na pesa toka serikali kuu.

Geremanus Byabusha – Diwani kata Kayanga

Bwana Byabusha amezitaja changamoto ambazo amekutana nazo kwa kipindi cha robo ya mwaka 2021 yaani kuanzia mwezi January hadi mwezi March na kuahidi kuzishughulikia kwaajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Geremanus Byabusha akieleza changamoto