Karagwe FM

Chanzo cha maji Katoke hatarini kutoweka

1 May 2021, 7:09 pm

Chanzo cha maji cha Katoke kilichopo katika kitongoji cha Ruzinga kata ya Bugene wilayani Karagwe,kipo hatarini kutoweka kutokana na baadhi ya wafugaji wa ng`ombe kukigeuza kuwa eneo la kunyweshea mifugo yao.

Wakazi wa kitongoji hicho wameieleza Radio Karagwe Sauti ya Wananchi kadhia hiyo ilipofika katika chanzo hicho cha kwa shabaha ya kuona maendeleo yake.

Chanzo cha maji Katoke kata ya Bugene wilayani Karagwe

Chanzo cha maji cha Katoke kinawahudumia sehemu ya wakazi wa vitongoji vya Ruzingz na Bugene.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho , Steven Simon ,amewasisitiza wafugaji kuacha mara moja kunyweshea ng`ombe katika hicho.

Mmoja wa wakazi wa Bugene anayetegemea chanzo cha maji Katoke

Kadhalika,mwenyekiti huyo ,amewataka wafugaji kunyweshea ng`ombe wao katika chanzo cha maji cha Nyabayamba ambacho kilitengwa kwa zoezi hilo.