Karagwe FM

DC Mwilla ashiriki kuondoa maji kwenye makazi ya watu

27 April 2021, 5:55 pm

Baada ya nyumba kadhaa na barabara za mitaa kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Missenyi, leo April 27,2021 Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denisi Mwila ameshirikiana na wananchi kuzibua mitaro na mifereji ya maji iliyoziba nakusababisha maji kujaa

Kitendo cha Mkuu wa wilaya kushirikiana nao katika kipindi hiki ambacho wananchi wamesema ni kigumu wamempongeza na kumshukuru kwa kutafuta wadau mbalimbali wanaoendelea kusaidia kufanikisha zoezi la kuondosha Maji yaliyojaa kwenye makazi ya watu na barabara za mitaa

Mkuu wa Wilaya Missenyi akiongea baada ya zoezi lakuzibua mitaro amewapongeza wananchi kwa jinsi walivyojitokeza kwa wingi kufanikisha zoezi Hilo

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denis Mwilla akiongea na mwandishi wetu

Mbali na Wananchi Mkuu wa Wilaya amewashukuru Kagera Sugar kwakutoa msaada wa nguvu kazi,Shirika na Redcross na WorldVision kwakupitia watu 44 walioko kwenye kambi ili kuwasaidia pia amemshukuru Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mwl Charles Katto na Katibu wa CCM Wilaya Missenyi Emmanuel Alex kwa msaada wao wa hali na mali