Zimamoto na Skauti
Karagwe FM

Jeshi la zimamoto laungana na Skauti kukabili moto.

20 April 2021, 9:26 am

Jeshi la zimamoto na uokoaji wilayani Karagwe limeungana na Skauti wilayani humo ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiteketeza mali za watu na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Picha ya pamoja Skauti, Jeshi la Zimamoto na Dc Karagwe

Staff Sergeant Peter Mbale ni Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji wilaya Karagwe amesema uzinduzi wa Programu hii ya kufanya kazi na Skauti ni utekelezaji wa agizo la Jeshi hilo kwa Nchi nzima,Kwa wilaya Karagwe uzinduzi umefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Sauti ya staff Sergeant Peter Mbale.

Mwalimu Lameck Kinyina ni Kamishina wa Skauti wa wilaya Karagwe amesema baada ya Muungano huo,wanakusuduia kuzielimisha shule za Sekondari 30,za Msingi 108 juu ya namna ya kupunguza majanga ya moto na kufanya uokoaji.

Lameck Kinyina (Kamishina wa Skauti wa wilaya Karagwe)

Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheluka ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa programu ya muungano wa Jeshi la zimamoto pamoja na Skauti wilayani humo.Amesema Muungano huo utakuwa na tija kwa jamii kama utafanya kazi kwa weledi na kutanguliza nidhamu.

DC Karagwe – Godfrey Muheluka