Barabara mbovu
Karagwe FM

Wananchi walia na ubovu wa Barabara.

17 April 2021, 5:21 pm

Wananchi wa kitongoji cha Karundu kata ya Bugene wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameiomba Halmashauri ya wilaya Karagwe iwatengenezee barabara za kitongoji hicho kwani wao wamejitolea bila kupata msaada mpaka wamechoka.

Baadhi ya wananchi wa Karundu wakiwa katika kikao hicho

Wananchi hao wamebainisha kero hiyo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho April 16,2021.

Baadhi ya viongozi walioshiriki mkutano April 16,2021.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho ,Pius Paulo amewahakikishia wananchi hao kuifikisha kero hiyo kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini ( TARURA )katika wilaya ya Karagwe ili waifanyie kazi na kuondoa changamoto zilizoko ambazo ni chanzo cha kukwamisha maendeleo.

Na mwandishi wetu Edson Lameck