Karagwe FM

” Ukikutwa na Sukari ni kesi ya Uhujumu Uchumi”

16 April 2021, 11:35 am

Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheluka amesema serikali wilayani Karagwe mkoani Kagera itaanzisha msako katika maduka yote wilayani humo kwa lengo la kuwakamata wafanyabiashara wote wanaosambaza na kuuza Sukari Nchini iliyotoka Nchi jirani ya Uganda bila kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kufungwa katika mifuko ya sukari ya kiwanda cha Kagera Sugar.

kulia ni Dc Karagwe Godfrey Muheluka.

Bwana Muheluka ametoa maagizo hayo April 15, 2021 wakati alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari ofsini kwake.Amesema msako huo utaanza rasmi April 16 mwaka huu na kwamba wote watakaokamatwa watafunguliwa kesi ya Uhujumu uchumi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheluka.