Karagwe FM

Kitendawili chateguliwa Kyenjubu.

16 April 2021, 9:32 pm

Wananchi walionunua viwanja eneo la Kyenjubu Missenyi Mkoani Kagera wako mbioni kukabidhiwa viwanja vyao ili waviendeleze

Mtaa wa Kyenjubu Misenyi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Innocent Mukandala amesema kuwa shughuli yakutengeneza barabara iliyokuwa imekwamisha zoezi lakukabidhi wananchi viwanja vyao inaendelea vizuri nakwamba baadhi ya viwanja kwasasa vinafikika hivyo akatoa wito kwa wale waliokamilisha malipo wakabidhiwe viwanja vyao  ili waviendeleze

Amesema kuwa wale ambao viwanja vyao havijafikiwa na barabara waendelee kusubiri mpaka Mkandarasi atakapokamilisha kutengeneza barabara zote nao watakabidhiwa “Kama kuna mwanachi amekamilisha malipo na kiwanja chake kinafikika kwasasa aje akabidhiwe ili akiendeleze hazuiliwi” amesema Mukandala.

Barabara za Kyenjubu- Misenyi zikikarabatiwa