Karagwe FM

Miradi 19 yalamba Milioni 250.

15 April 2021, 1:25 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Innocent Mukandala amesema kuwa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango leo alhamisi tarehe 15 April 2021 imeanza ziara ya siku 2 ya kufuatilia na kukagua miradi ya Maendeleo 19 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250

Mukandala ametaja baadhi ya miradi itakayokaguliwa kuwa ni pamoja na shamba la Kahawa lenye Miche 9,000 lililoko Mushasha,Ujenzi wa vyumba vya madarasa,Bweni na maabara katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari, Ujenzi wa zahanati Kikukwe pamoja na matengenezo ya barabara za Mradi wa viwanja Kyenjubu

Kabla yakuanza ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Diwani wa Kata Kyaka Projestus Tegamaisho amesema kuwa lengo lakukagua miradi hiyo nikuona thamani ya fedha (Value for money),hali ya utekelezaji ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora wenye viwango vinavyotakiwa.

Sauti ya M/Halmashauri ya (W) Misenyi Projestus Tegamaisho

Madiwani wanaounda Kamati ya fedha ni Projestus Tegamaisho (Kyaka),Msafiri Nyema (Ishunju), Yusuf Ahamada (Kassambya),Henry Bitegeko (Gera),Richard Mbekomize (Kakunyu), Doris Kyombo,Reticia Paschal (Kilimilile),Paulina Kajula,Willy Mutayoba (Kitobo).

Wajumbe wa Kamati ya FUM ( shambani Kwa Muzamiru Suleiman )