UJENZI
Karagwe FM

Kata kujenga zahanati na Sekondari.

14 April 2021, 9:31 pm

Wananchi wa kitongoji cha Bugene Kata ya Bugene Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera wametakiwa kushiriki kikamilifu ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya sekondari na Zahanati kwenye kata hiyo vinavyo tarajiwa kujegwa hivi karibuni.

Wananchi wakiandaa tofali kwaajili ya ujenzi
Baadhi ya wanachi wa kata Bugene.

Diwani wa kata hiyo Mugisha  Anselim amebainisha haya kupitia  kwenye mkutano wa kitongoji uliowakutanisha viongozi wa kata na wananchi   ambapo amesema kuwa utekelezaji wa mpango huu unatokana na uwepo wa ongezeko la   wananchi  swala linalosababisha uhitaji wa shule ya sekondari pamoja na zahanati kwaajili ya kupambana na changamoto zilizoko kwa sasa.

Sauti ya Diwani wa kata Bugene Mugisha Anselim