Nyaishozi Fc
Karagwe FM

Nyaishozi fc kufa kupona ligi ya mabingwa.

13 April 2021, 7:17 pm

Timu ya mpira wa miguu Nyaishozi ya wilaya Karagwe mkoani Kagera imejipanga vyema kuhakikisha inasonga mbele katika hatua inayofuata kwenye ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCLFinals 2021).

DC Karagwe – Godfrey Muheluka akikabidhi michango kutoka kwa wadau (Milioni Nne.)
Sauti ya Dc Karagwe Godfrey Muheluka.

April 12 mwaka huu timu hiyo ambayo ni Mshindi wa mkoa Kagera imesafiri kutoka wilayani Karagwe Kuelekea mkoani Lindi ili kushiriki Ligi hiyo itakayozikutanisha jumla ya timu 8 katika uwanja wa Ilulu.

Kwa mujibu wa TFF Ligi hiyo inatarajia kuanza April 16 – 25,2021.Timu zinazoshiriki zinatakiwa kuwasili kituoni April 14, 2021.

Nyaishozi Fc wakiwa na Mbunge wa Karagwe Bashungwa