WAZIRI BASHUNGWA
Karagwe FM

Ni Tv za online kwanza

8 April 2021, 12:50 pm

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza TCRA kuzifungulia TV za mtandaoni zote (Online TV) ambazo zilifungiwa ikiwa utekelezaji wa maelekezo ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa April 06 ,2021 wakati akiwaapisha Makatibu wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali.

Waziri Bashungwa ametoa maelekezo hayo April 07, 2021 katika Makumbusho ya Taifa Dar es salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kabla ya hafla uzinduzi wa filamu ya kumbukumbu ya kuenzi maisha na Kazi zilizofanywa na Hayari Dkt. John Pombe Magufuli, Aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Bashungwa ameendelea kutoa ufafanuzi kwa upande wa magazeti ambapo ameeleza kuwa yalifungiwa kwa sheria huku akitoa wito kwa wamiliki kufika ofisni kwake ili kuangalia nini kilipelekea kufungiwa na nini kifanyike ili na wafunguliwe na kurudi katika utaratibu wa kutoa habari kwa mujibu sheria na utaratibu

“Kwa upande wa haya magazeti ambayo kwa sababu zotozote yalifungiwa, Sheria ndizo zilitumiwa kuwafungia ndo maana nikasema haya tutaenda nayo case by case, Ofisi yangu iko wazi, waje tuangalie nini kilipelekea kufungiwa na nini kifanyike ili warudi kwenye utaratibu wa kuendesha Vyombo vya Habari kwa mujibu wa sheria na kanuni za uendeshaji wa Vyombo vya Habari” ameeleza Bashungwa

Sauti ya Waziri Bashungwa

На нашем сайте уже вышла статья о том как получить мелбет бездепозитный бонус