Kahama FM

BASI LA RUKSA CLASS LAUA WATU WATATU NA KUJERUHI WANNE KAHAMA

May 25, 2022, 11:00 am

Watu watatu wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa  katika ajali ya Basi la Abiria kampuni ya RUKSA CLASS baada ya kupinduka katika Kijiji cha Kayenze halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando amesema ajali hiyo imetokea  juzi majira ya saa sita mchana, ambapo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hilo kushindwa kulimudu basi hilo.

Kyando amebainisha kuwa waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Doris Machibya[16},Masudi Juma{35},na Halima Masolwa[50}, ambapo miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya halmashauri ya manispaa ya Kahama,huku majeruhi wakiendelea na matibabu.