dr kitima
Kahama FM

DR KITIMA:Wanaume na wanawake wote wana haki ya Kuishi,Acheni mauaji.

February 14, 2022, 3:31 pm

Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC) Dr Charles Kitima

DAR ES SALAAM

Jamii imetakiwa kuelewa kuwa wanaume na wanawake wote wana haki sawa ya kuishi na kufanya shughuli zozote zilizo halali na kwamba wanaume waache tabia ya unyanyasaji na mauaji yanayofanywa dhidi ya  wanawake.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki hii  na Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania (TEC) Dr Charles Kitima katika mdahalo uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu haki za wanawake na mauaji  ya Kikatili nchini  Tanzania.

Sauti ya Dr Charles Kitima

Katika hatua nyingine Dr Kitima Ameongeza kuwa nchini Tanzania kwasasa mauji ya wanawake yanaondelea ni dhana potofu kuwa mwanamke ni chombo cha mwanaume na kwamba jamii imesahau kuweka haki za binadamu katika mila na desturi.

Sauti ya Dr Kitima

Naye Mwakilishi kutoka ofisi ya Mufti mkuu wa baraza la waislamu Tanzia Sheikh Swed Twaibu Swed ametoa wito kwa vyombo vya dola na mabaraza ya usuluhishi kumaliza kesi kwa wakati hasa za Mirathi ili kuondoa hali ya wanawake kuchanganyikiwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Sauti ya Sheikh Swed Twaibu

Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya haki za binadamu na Utawala bora Tanzania Dr Fatma Khalfan ameitaka jamii kujitokeza kupaza sauti inapoana unyanyasaji na kuacha tabia ya kukaa kimya na kusema hayo ni mambo binafsi.

Sauti ya Dr Fatma Khalfan

Mdahalo huo uliofanyika kwa njia ya mtandao kuhusu haki za wanawake na mauaji  ya Kikatili nchini  Tanzania umeratibiwa na Shirika la Freedom House na Kuhudhuliwa na watu zaidi ya mia moja.