kahama
Kahama FM

POLISI KAHAMA: Watembea kwa Miguu acheni Madoido kwenye vivuko vya Pundamilia.

January 5, 2022, 11:49 am

Askari wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Hezron Gudaga

Jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga limewataka watembea kwa miguu kuheshimu alama za barabarani wakati wa kuvuka hasa eneo la pundamilia na kuacha tabia ya kutembea kwa mizaha eneo hilo.

Wito huo umetolewa leo askari wa usalama barabarani Hezron Gudaga wakati wa mahojiano katika kipindi cha Ukurasa mpya kinachorushwa na Redio Kahama iliyopo manispaa ya Kahama.

Gudaga amesema kuwa wapo watembea kwa mguu hawaheshimu alama za pundamilia kwa kuvuka wakiwa wanacheza na wengine hawaangalii magari wala hawasimami pembeni ya barabara.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa alama ua Pundamilia siyo kigezo cha mtembea kwa miguu kuvuka atakavyo bali anatakiwa afuate taratibu ikiwa ni pamoja na kuangalia kushoto na kulia kabla hajavuka barabara.

Sambamba na hayo Gudaga ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria na taratibu ikiwa ni pamoja na kupunguza mwendo kwenye alama za Pundamilia  na kusimama pale ambapo alama za usalama barabarani zinawataka kufanya hivyo zikiwemo taa za barabarani.

Pedestrian crossing the zebra road. Traffic Laws.

Awali wakichangia mjadala huo baadhi ya wasikilizaji wa  Redio Kahama wamelipongeza jeshi la Polisi manispaa ya Kahama kwa kuanzisha utaratibu wa Junior Patrol unaowawezesha wanafunzi kuvushana barabarani katika shule zilizopo maeneo ambayo magari yanapita.

Wameongeza kwa kuliomba Jeshi la Polisi na wahusika wengine kurudia kuchora na kuweka upya michoro ya alama za barabarani zilizofutika ili kuwasaidia watembea kwa miguu kuzitambua alama hizo.

Mfano wa njia ya Junior Patrol inayotumiwa na wanafunzi kujivusha wenyewe kwa wenyewe barabarani.