isaka jana
Kahama FM

Kahama: Serikali wilayani Kahama imekabidhiwa Madarasa 247 yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6.

December 16, 2021, 12:50 pm

isaka jana
mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekabidhiwa Madarasa 247 yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 yaliojengwa kwa fedha za fedha za Uviko 19.

Akikabidhiwa madarasa hayo leo Mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA na  wakurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kahama, Ushetu na Msalala amesema kuwa kazi imefanyika ndani ya mwezi moja, na kukamilisha kwa wakati madarasa hayo ambapo amewapongeza wakurugenzi kwa kukamilisha ujenzi huo.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala CHARLES FUSI, mkurugenzi wa Ushetu LIMO MWAGENI kaimu mkurugenzi manispaa ya kahama CLEMENT MKUSA wamesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa uaminifu ili kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza watakaoanza masomo mwaka 2022.

Sauti ya mkuu wa wilaya za wakurugenzi(Msalala, Kahama Manspaa na Ushetu)

Naye Afisa elimu msingi halmashauri ya manispaa ya Kahama HAMIDA KAGANDA amesema madarasa hayo yatasaidia wanafunzi kusoma vizuri kutokana na ubora wa madarasa hayo, pamoja na kuondokana na mlundikano wa wanafunzi darasani.

Afisa elimu Hamida Kadanga