isaka jana
Kahama FM

KAHAMA:Dc amsimamisha kazi Mwenyekiti wa kijiji aliyekataliwa na wananchi.

November 9, 2021, 9:50 am

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga

Wakazi wa  kijiji cha Butondolo kata ya Isaka jana, halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga  wamemkataa mwenyekiti wa kijiji hicho, Mange Shilinde baada ya kubatilisha na kuhamisha ujenzi wa zahanati ya kijiji katika kitongoji cha Seseko bila idhini yao, pamoja na kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwatoza faini ya ng’ombe  wanaobainika kupinga maamuzi yake.

Uamuzi huo umekuja baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kubatilisha maamuzi ya mkutano mkuu  wa kijiji ulioketi mwaka 2016 uliopendekeza zahati ya kijiji hicho ijengwe katika kitongoji cha Seseko ili kutoa fursa kwao kupata huduma za matibabu kwa ukaribu.

Nkwabi Bucheyebi na Salu Lukelesha ni wakazi wa kijiji hicho wakapaza sauti kwa serikali kuhusiana na mgogoro huo uliosababisha shughuli za maenedeleo katika kijiji hicho kukwama kwa muda mrefu kutokana na wananchi kugoma kuchangia michango ya ujenzi wa zahanati hiyo.

Sauti za wananchi wa Kijiji cha Butondolo.

Mihambo Kizito ameelezea namna walivyokabiliana na tatizo hilo huku huku diwani wa kata hiyo Paschal Mlingito akiiomba serikali kuutatua mgogoro huo.

Sauti ya Mtendaji wa kata na Diwani

.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Mange Shilinde amekata tuhuma zilizotolewa dhidi yake huku mkuu wa wilaya ya kahama Festo Kiswaga amelazimika kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili na kuagiza uongozi wa kijiji hicho kuteua mwenyekiti mwingine wa muda ili kusimamia maendeleo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Butondolo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama.