Kahama FM

KAHAMA:RUWASA YAKUTANA NA WADAU WA MAJI NA VYOMBO VYA WATOA HUDUMA ZA MAJI;

October 31, 2021, 4:38 pm

Katibu tawala wilaya ya Kahama TIMOTHI NDANYA(katikati)

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kutumia maji yanayotokana na vyanzo vya uhakika vilivyothibitishwa kwa ubora na RUWASA ili yawe salama katika afya zao pamoja na kuwataka viongozi kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kwa wakati.

Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya ya Kahama TIMOTHI NDANYA katika kikao cha (RUWASA) na wadau wa maji mjini Kahama, ambapo amesema kuwa wananchi wanapaswa kutumia maji hayo ambayo ni salama ili kuepukana na magonjwa mbalilimbali.

Kwa upande wake kaimu meneja wa RUWASA PASCHAL MNYETI amesema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma za maji kwa wilaya ya Kahama imefikia 64.4% sawa na zaidi ya watu laki nne wanaoishi vijini, huku ikiwa na visima vifupi 471 na virefu 27 vinavyofanya kazi katika wilaya hiyo.

Nao, wananchi waliohudhuria kikao hicho cha wadau wa maji na wasimamizi wa miradi ya maji wameiomba RUWASA kutatua changamoto wanazokutana nazo wakati wa kuwahudumia wananchi ikiwemo bei, ili kila mwananchi awe na uwezo wa kumudu kutumia maji hayo.

Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kahama kila mwaka hufanya mikutano miwili na wadau wa maji ili kujadili namna gani ya kuendelea kuboresha huduma ya maji kwa kutumia miradi yao mbalimbali ya maji.