Kahama FM

KAHAMA:RUWASA YATAKIWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI MBALIMBALI KWA WAKATI.

October 31, 2021, 4:25 pm

Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kila mwananchi apate maji pamoja na kuanza ujenzi wa usambazaji wa maji pindi wanapopata fedha za miradi.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA katika ziara yake ya siku mbili na kamati ya ulinzi na usalama katika kukagua miradi ya maji katika halimashauri za Msalala na Ushetu, ambapo ameipongeza RUWASA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwataka kukamilisha miradi ambayo bado haijakamilika.

Kwa upande wake meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama MADUHU MAGILI amesema kuwa katika halmashauri ya Msalala wamekamilisha takriban miradi minne.

Nao wananchi wa halmashauri ya msalala wakizungumza na kahama fm wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapeleka  huduma hiyo ya maji.