kahama jogging
Kahama FM

Kahama Jogging yajipanga kuwakabili Shinyanga Jogging Jumapili Oct 17.

October 10, 2021, 1:53 pm

Wanawake wa Kahama Jogging wakiwa katika mazoezi ya mbio za Magunia.

Kuelekea Mashindano ya Michezo mbalimbali itakayofanyika uwanja wa Manispaa  Kahama Jumapili ya October 17 club ya ya mazoezi ya Kahama Jogging imeanza maandalizi ya kuwakabili Club ya Michezo kutoka Shinyanga itwayo Shinyanga Jogging.

Akioongea na Kahama Fm mara baada ya mazoezi ya asubuhi ya leo Mwenyekiti wa Kahama Jogging Hussen Salumu amesema kuwa Kahama Jogging imejipanga kushinda michezo yote kwani washiriki wamejitoa kwa moyo wote kuhakikisha wanashinda katika michuano hiyo.

Salumu amesema kuwa wanawatambua Shinyanga Jogging kwa muda mrefu na kwamba mashindano ya Jumapili wasitegee ushindi wowote kwani mazoezi wanayoendelea nayo ni makali yakuhakikisha ushindi unabaki Kahama.

Akielezea mazoezi yaliyofanyika leo Katibu wa Kahama Jogging Yusuph Makombe amesema kuwa leo wamekimbia umbali wa km 10 kukimbia kwenye magunia na kuvuta kamba sanjali na kufanya mazoezi ya viungo.

Kahama Jogging wakiwa katika mazoezi ya Km 10 mapema asubuhi ya leo.

Nao baadhi ya wanachama wa Kahama Jogging Steve Cleophace na Lubango Yusuph wamesema kuwa wamejipanga vizuri kushindana na Shinyanga Jogging na kwamba mazoezi yote wanayotolewa na walimu wanayazingatia huku wakitoa salamu kwa wapinzani wao kujiandaa kikamilifu.

Kahama Jogging  inatarajia kuwakaribisha Shinyanga Jogging siku ya jumapili October 17 katika uwanja wa Manispaa Kahama kushindana michezo mbalimbali ikiwemo Mbio za kawaida na mbio za magunia,Kuvuta kamba,Mpira wa miguu,Mpira wa pete pamoja na michezo mingine.

Mazoezi ya mbio ya Mita 100 yakiendelea katika uwanja wa manispaa Kahama.