kahama
Kahama FM

KAHAMA:Wananchi wa Kata ya Malunga waanza ujenzi wa Shule ya Sekondari.

September 20, 2021, 4:30 pm

Wananchi wa Kata ya Malunga Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wameanza zoezi la ujenzi wa shule ya Sekondari Malunga ili kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu.

Wakizungumza na Kahama fm baadhi ya wananchi hao wamesema baada ya kukamika shule hiyo ya Sekondari Malunga iwatasaidia wanafunzi wa kata hiyo kutotembea umbali mrefu  kwenda shuleni.

Aidha wananchi hao wamewaomba wananchi wengine pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki katika ujenzi wa shule hiyo.

Wananchi wa kata ya Malunga.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Malunga JOSEPH MIPAWA amesema uwepo wa shule hiyo utapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya sekondari Kishimba.

Diwani wa kata ya Malunga

Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Malunga OMARY ABDALLAH amesema wananchi wameamua kuanza ujenzi wa shule hiyo kwa kuwa wanahitaji maendeleo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Malunga.

Ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari Malunga unatarajiwa kukamilika mwezi January 2022.