Kahama FM

KAHAMA:VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA VIMETAKIWA KUIGA MFANO WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA(KACU).

September 15, 2021, 3:03 pm

Waziri wa kilimo Profesa Adolfu Mkenda

Serikali imevitaka vyama vikuu vya ushirika nchini kuiga mfano wa chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) kwa kununua pamba na kuingia kwenye mnyororo wa thamani.

Waziri wa kilimo profesa ADOLF MKENDA ametoa wito huo leo alipotembelea kiwanda cha chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU), kilichopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

PROF. MKENDA amekipongeza chama hicho kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima kutoka bei elekezi ya shilingi 1050 hadi sh 1700 pamoja na kununua pembejeo za kilimo cha zao la pamba na kuzigawa kwa wakulima.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama, FESTO KISWAGA amesema kwa mwaka huu wilaya ya Kahama inatarajia kuzalisha zaidi ya kilo milioni 50, ambapo amesema serikali itahakikisha inasimamia uzalishaji huo.

Naye mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) EMMANUEL CHERAHANI ameishukuru serikali kwa kutoa mbegu za pamba pamoja na dawa, zenye thamani ya shilingi bilioni 26 na million 500.

Chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU) kwa mwaka huu kimeweza kununua pamba, ambapo hadi sasa kimenunua zaidi ya kilo milioni 3 na laki 3.