Kahama FM

KAHAMA: MLINZI AUAWA KWA KUCHOMWA NA KISU GUEST.

September 13, 2021, 11:14 am

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP GEORGE KYANDO

Mlinzi Kampuni ya Ulinzi ya Mast Holding aitwaye STEVEN FELICIAN SAMANDARI (25) ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa Bar kwa ajili ya mapenzi Mjini Kahama.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP GEORGE KYANDO kwa vyombo vya habari, tukio hilo limetokea Septemba 11,mwaka huu majira ya saa nane usiku katika mtaa wa Nyahanga kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.

 “Mlinzi huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi”,amesema.

“Chanzo cha tukio hilo ni kufuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi. Eneo la tukio kimeokotwa kisu kikiwa tumboni. Mbinu iliyotumika ni kuchoma kisu tumboni”,amesema Kamanda Kyando.

Kamanda KYANDO amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aitwaye FATUMA JUMA CHARLES (22), mhudumu wa bar kwa uchunguzi.