Kahama FM

Mwanamke auawa akituhumiwa kuwa mchawi.

September 11, 2021, 4:32 pm

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la MWALU CHARLES (45) mkazi wa kijiji cha Shilabela kata ya Ulewe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali huku chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha Shilabela, kata ya Ulewe, tarafa ya Mweli ,wilaya ya kipolisi Ushetu, wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga.

Sauti ya kamanda George Kyando

KYANDO Amesema tayari watuhumiwa watatu wamekamatwa, huku akibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia unaochochewa na imani za kishirikina.

Sauti ya kamanda George Kyando