Kahama FM

MFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB ANUSURIKA KUFA KWA KUPIGWA NA MUME WAKE.

September 11, 2021, 4:57 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Debora Rwekwama (34) mkazi wa Bushushu Mjini Shinyanga amefanyiwa ukatili kwa kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aitwaye JACOBO MWAJENGA (35) kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9 mwaka huu, usiku katika mtaa wa Bushushu, Manispaa ya Shinyanga.

INSERT: NKYANDO

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

KYANDO amesema baada ya kufanya tukio hilo, MWAJENGA alimbeba mke wake akiwa amezimia na kumbeba kwenye gari yao na kumpeleka hadi katika kituo cha Polisi Kahama.

Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi na kwamba tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa wa tukio hilo.

Ameeleza kuwa hali ya majeruhi ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama.

Kamanda KYANDO amesema hivi sasa kuna matukio mengi ya vifo vinavyotokana na wivu wa mapenzi, hivyo ametoa kutoa wito kwamba wananchi wasijichukulie sheria mkononi,waende kwa viongozi wa dini,serikali au vyombo vya dola kutafuta suluhisho.