mobisol
Kahama FM

KAHAMA:Mobisol yawataka Wananchi kutumia umeme jua kujiletea maendeleo.

August 29, 2021, 2:08 pm

Banda la MOBISOL katika maonyesho ya Biashara Kahama.

Na William Bundala

Kahama

Kampuni ya usambazaji wa huduma za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua (Mobisol) wilayani Kahama mkaoni Shinyanga imewataka wananchi wilayani Humo kutumia nishati hiyo ikiwa njia mbadala ya kupata nishati ya umeme yenye gharama nafuu ili kujiletea Maendeleo.

 Hayo yamebainishwa leo na Meneja eneo wa kampuni hiyo Alex Kasangaya wakati akiongea na Kahama fm kwenye kilele cha Maonyesho ya biashara yanayofanyika kwenye uwanja wa taifa manispaa ya  Kahama.

Kasangaya amesema kuwa Mobisol Tanzania imedhamiria kuwapa huduma bora wakazi wa Kahama na kwamba wajipanga kuwafikia watu wote mijini na vijijini katika kufikisha umeme mbadala wa nishati ya jua kwa bei nafuu.

Sambamba na hayo Kasangaya ametoa wito kwa wananchi wote kufika katika banda lao lilipo uwanja wa Taifa Kahama ili kupata elimu na kutambua umuhimu wa nishati ya jua (Mobisol) katika kujikwamua kiuchumi.

Mitambo ya Mobisol ambayo Utaipata ukiwa katika Ofisi zozote nchiniTanzania.

Katika hatua nyingine Kasangaya ameongeza kuwa Mobisol Kahama inatoa mitambo ya Sola kwa mkopo kuanzia mtambo wa milioni laki saba na thelathini na nne hadi milioni tatu laki nne na themanini na sita.

Kwa upande wake meneja tawi wa Mobisol Kahama Mohamed Said amewataka wateja wote wanaomiliki mitambo ya Mobisol kuendelea kutumia mitambo ya nishati ya Umeme bila hofu kwani bado wana midhamana mikubwa na kwamba waendelee kuwahamasisha wateja wengine ili wazidi kupata bonus ikiwa ni Pamoja kupata punguzo la malipo ya mwezi .

Maonyesho ya biashara Kahama yaliyobebwa na kauli mbiu Michezo,Afya na Biashara yameanza tangu August 23 na yanatarajia kuhitimishwa kesho August 29 na Mgeni rasmi Waziri wa habari utamaduni na Michezo Mh Innocent Bashungwa.