TUNEL
Kahama FM

KAHAMA: Watanzania watakiwa kuwa wazelendo kutumia bidhaa za Nyumbani.

August 29, 2021, 3:12 pm

Afisa mauzo wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa Vinywaji ya TUNEL Incorporation Limited ya mjini Kahama Semmy Msangi.

Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo kwa kutumia bidhaa za nyumbani ikiwa ni njia ya kuongeza pato la taifa Pamoja na kuweka hamasa kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza katika biashara mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo na Afisa mauzo wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa Vinywaji ya TUNEL Incorporation Limited ya mjini Kahama Semmy Msangi katika kilele cha maadhimisho ya Maonyesho ya Biashara mjini yaliyokutanisha wajasiliamali wakubwa na wadogo.

Msangi amesema kuwa kampuni ya kizawa ya TUNEL ya mjini Kahama imedharamia kuleta mapinduzi ya huduma ya vinywaji kwa kuuza vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi ndani na nje ya Tanzania.

Sambamba na hayo Msangi amesema kuwa vinywaji vyote vinategengezwa kwa mazao ya Tanzania kama vile Tangaziwi,Ndizi,Mananasi Pamoja na miwa na kuwataka wananchi kulima mazao hayo kwa wingi na kupata soko la ndani.

Kwa upande wake Afisa mahusiano masoko wa kampuni ya TUNEL Martha Lumelezi amesema kuwa kampuni yao imeajili watu Zaidi ya watu 50 na kwamba kampuni yao imedhamiria kuleta mapinduzi ya viwanda kwa kuleta bidhaa bora na zinazopendwa na watanzania.

Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya TUNEL Incorporation Limited .

Maonyesho ya biashara Kahama yaliyobebwa na kauli mbiu Michezo,Afya na Biashara yameanza tangu August 23 na yanatarajia kuhitimishwa kesho August 29 na Mgeni rasmi Waziri wa habari utamaduni na Michezo Mh Innocent Bashungwa.