TANZIA
Kahama FM

TANZIA:Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila afariki dunia.

August 23, 2021, 7:36 am

David Nkulila enzi za uhai wake

Mstahiki Meya wa Manispaa 1ya Shinyanga David Mathew Nkulila ambaye ni Diwani kata ya Ndembezi David Nkulila amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 23,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu kutokana na kuugua kwa muda mrefu.

Msiba upo nyumbani kwake mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi jirani na Kanisa la Moravian.

Nkulila ambaye pia amewahi kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga ametumikia nafasi ya Meya kwa kipindi cha mwaka mmoja na udiwani kata ya Ndembezi kwa zaidi ya miaka 10.

R.I.P Nkulila