msumba
Kahama FM

MSUMBA:Wana Kahama endeleeni kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yetu.

August 23, 2021, 8:49 am

ANDERSON MSUMBA

Wananchi katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu mbalimbali za manispaa  pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali kwa manufaa ya wanakahama.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya kahama ANDERSON MSUMBA amesema kwa kushirikiana na wananchi pamoja na watendaji, manispaa imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapatao kutoka shilingi billion 3 kwa mwaka 2016 hadi mwaka 2021 imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 9.

Sauti ya Msumba

MSUMBA amesema wamefungua mfumo kidhibiti udanganyifu kwenye ukusanyaji wa mapato ambao kwa siku wanaweza kuangalia kiasi gani cha mapato yanaingia, pamoja na kujua walipa kodi katika maeneo yote ya manispaaya kahama.

Msumba akisisitiza jambo

Hata hivyo, amesema kuwa wananchi wanaolipa kodi wanahaki ya msingi ya kufahamu juu matumizi ya kodi zao, huku akiwataka wananchi wa manispaa ya kahama kuijenga kahama kwa kulipa kodi pasipo kushurutishwa.