kahama
Kahama FM

KAHAMA:Wakulima wa pamba waomba kupatiwa Elimu ya Kilimo Hai.

August 17, 2021, 4:16 pm

Viongozi wa vyama vya Msingi vya Tumbaku na Pamba

KAHAMA

Wakulima wa zao la Pamba wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameiomba kampuni ya utengenezaji wa nyuzi New Tabora Textile kuwapa elimu ya uzalishaji wa pamba usiotumia Dawa na mbolea nyingi katika uzalishaji(Kilimo hai)

Ombi hili limetolewa na wakulima wa Pamba katika kikao cha viongozi wa vyama vya msingi vya Tumbaku na Pamba kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa KACU.

Wakulima hao wamesema kuwa wapo tayari kufanya mabadiliko ya kilimo kutoka kilimo duni kwenda kilimo cha kisasa ila changamoto kubwa inayowakabili ni elimu ya namna ya kulima kisasa bila kutumia mbolea nyingi na madawa hatarishi.

Sauti za wakulima wa Pamba wakiomba kupew elimu.

Akijibu maombi hayo mtaalamu wa Kilimo hai Tanzania Shiju Kuttappan amesema kuwa kilimo hai hakikatazi matumizi ya mbolea na dawa bali kinafundisha ni aina gani ya pembejeo utumie na kwamba watawapa elimu ili kufikia malengo.

Sauti ya Mtaalamu wa kilimo Hai Shiju Kuttappan.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama kikukuu cha ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani amesema kuwa wao wapo tayari kupokea elimu ya Kilimo Hai na kwamba kilichobaki wataalamu wafike mapema kutoa elimu kwa wakulima kwani mkakati ni kuzalisha pamba safi na nyingi katika msimu ujao.

Mwenyekiti wa chaama kikuu cha wakulima Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani.
Sauti mwenyekiti wa chama kikukuu cha ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani

Katika msimu uliopita wa mwaka jana Wilaya ya Kahama ilizalisha Jumla ya kilo laki 7 na tano 571 elfu  za pamba zilizalishwa na kuuzwa kwa bei ya Shilingi 920 na katika msimu huu mpya wa pamba matarajio ni kuzalisha kilo Milioni 3 na laki 6 kwa bei ya Shilingi 1100 hadi 1300.