Kahama FM

Wanaume wilayani Kahama washauriwa kutoa taarifa za ukatili.

July 7, 2021, 11:19 am

Wanaume wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameshauriwa kutoa taarifa za ukatili katika dawati la jinsia pindi wanapofanyiwa  ukatili na wenza wao, ili waweze kutatuliwa changamoto zinazowakabli katika jamii..

Wito huo umetolewa na KOPLO JOSEPH shayo wakati akizugumza na KAHAMA FM, ambapo amesema  wanaume wengi wamekuwa na mtazamo potofu kuwa dawati la jinsia ni kwa ajili ya wanawake.

SHAYO amesema tangu mwezi january mawaka huu hadi june zaidi ya wanaume 30 wamesikilizwa

Kwa upande wake afisa dawati la jinsia NINAEL KISAGASE amesema kutokana na ei mu inayotolewa na dawati hilo kwa sasa wanaume wengi wamekuwa wakitoa taarifa

Kwa upande wao baadhi ya wananchi katika manspaa ya kahama wametoa wito kwa wanaume kuwa wazi na kutambua kuwa wanahaki ya kutoa taarifa za ukatili.

Dawati la jinsia na watoto ni kitengo kilichopo ndani ya jeshi la.​polisi kinachoshughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia pamoja na unyasasaji dhidi ya watoto.