Kahama FM

kikundi cha vijana 10 chapatiwa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi millioni 50 kijiji cha Kakola kata Bulyanhulu.

July 7, 2021, 4:18 pm

Mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA

Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi millioni 50 kwa kikundi cha vijana 10 katika kijiji cha Kakola kata Bulyanhulu.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki hizo mkuu wa wilaya ya Kahama FESTO KISWAGA amesema serikali inaendelea kuhakikisha vijana wanapata ajira pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, ambapo amemtaka mbunge wa jimbo hilo IDD KASSIMU kutekeleza kile alichowaahidi wananchi na kuahidi huwa serikali ipo Pamoja naye.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Msalala IDD KASSIMU amesema katika kuhakikisha serikali inatatua changamoto za wananchi, jimbo limepokea kiasi cha shilingi billioni moja kwa ajili ukamilishaji wa hospitali ya ntobo, pia billioni 4, million 60 kwa ajili ya miradi ya maji katika jimbo hilo.

Naye, diwani wa kata ya Bulyanhulu,JOSEPH LUYOMBYA amesema katika kata hiyo kuna zaidi ya shilingi millioni 144 kwa ajili ya  vijana na wanawake iki kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha waendesha pikipiki (bodaboda) RAJABU ZEPHANIA pamoja na katibu wa kikundi hicho RAJABU MAGUNYA wameishukuru serikali kwa mkopo huo  usio na riba ambapo wataweza kujiendeleza kiuchumi pamoja na kupunguza changamoto walizokuwa nazo awali.

 

Pikipiki 20 zimetolewa kwa kikundi cha vijana 10 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kila halmashauri kutoa mikopo ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kuwezesha makundi mbalimbali ikiwemo vijana wanawake na walemavu.